Hili ni moja ya swali linalopendwa kuulizwa wakati wa usahili. Kumbuka kwamba kila swali unaloulizwa kwenye usahili linalenga kuonesha “a positive side of you” lakini hii haikupelekei kubadili udhaifu wako kuwa “strengths”.
Swali hili linalenga kupima uwezo wako wa kujitambua “Self Awareness”, uwezo na kiu yako ya kutaka kujifunza “Self Initiative and Eagerness to Learning” lakini pia uwazi “Honesty”. Mwajiri pia anataka kujifunza kuhusu mapungufu yako na ni kwa namna gani mnaweza mkashirikiana na kufanya kazi pamoja bila kupelekea changamoto zozote.
Unapojibu hili swali hili swali hakikisha mazuri yako yanafunika udhaifu wako. Mapungufu yasiwe na nguvu kuliko mazuri uliyokwisha kuyataja. Mapungufu utakayozungumzia yasiwe na uwezo wa kuathiri utendaji wako wa kazi unayoiomba. Kwahiyo hakikisha unaelewa vizuri kazi unayoiomba.
Yafuatayo ni mambo ambayo unaweza kufanya ili kujibu swali hili kwa ipasavyo:
Kuwa halisi (Be authentic): Hakikisha unazungumzia weakness zako. Usi”fake” mambo. Tumia mifano halisi kuhusu maisha yako (both personal and career wise).
Jikite kwenye juzi ambazo hazihusani moja kwa moja na kazi unayoomba (non-essential skills): Hskikisha unachagua skills ambazo hazitaathiri utendaji wako wa kazi unayoomba. Kabla ya kwenda kwenye usahili, andaa list ya weakneses zako na changua ambazo utazizungumzia kuendana na kazi uliyoomba.
Zingatia eneo la “experience” kama mojawapo ya sehemu za weaknesses: Hii ni hususani kwa wale junior professionals kama graduates n.k. Vilevile kama wewe ni mgeni kwenye tasnia flani unaweza kuelezea kuwa unahitaji kupata uzoefu kwenye industry nyingine. Hakikisha unaonesha kiu yako ya kutaka kujifunza.
Elezea namna ambavyo umekuwa ukipambana kurekebisha mapungufu yako: Mfano, kusoma vitabu, kuongea na watu wa industry yako, kusoma kozi mtandaoni n.k. Elezea jinsi ulivyokuwa awali na ulivyo sasa.
Acha kutumia cliches/ buzzwords: Mf. workaholic, perfectionist etc.: Haya hayakuelezei inavyotakiwa. Jielezee kwa kina katika namna ambayo anayekusikiliza atakuelewa au hatakuwa na maswali.
Jiamini: Elezea mapungufu yako kwa kujiamini bila woga. Kinachotakiwa ni kuwa uoneshe ni namna gani unavyozifanyia kazi kurekebisha.
Penda kusimulia zaidi: Ukitumia hadithi za maisha yako zitamsaidia anayekusikiliza kukuelewa kwa haraka. Zingatia kuonesha ni jinsi gani unavyofanya kazi kubadili mapungufu yako
Angalia mfano, jinsi ya kujibu, “Tell me about your weaknesses”.
“My greatest weakness is that I sometimes have trouble saying ‘no’ to requests and end up taking on more than I can handle. In the past, this has led me to feel stressed or burned out. To improve in this area, I use a project management app so I can visualize how much work I have at any given moment and know whether or not I have the capacity to take on more.”
Mifano zaidi imeandikwa katika chapisho hili Weaknesses for Job Interviews: 10 Example Answers.
Nimalizie kwa kusisitza, kujiandaa kabla, kuepuka kuzungumzia vitu vitakavyoathiri utendaji wako wa kazi unayoomba lakini pia kuonesha kuwa hujakubaliana na kuishi na hayo mapungufu yako bali unafanyia kazi kuyarekebisha vi vitu muhimu unapojibu swali la mapungufu/ udhaifu wako kwenye usaili.