Moja ya maswali waajiri wanayopenda kuuliza ni pamoja na kutaka kujua ni kiasi gani cha mshahara unachotegemea kulipwa kulingana na kazi unayoenda kuifanya. Swali hili linaulizwa siyo kwamba ni mtego lakini mwajiri anataka kujua kwamba mategemeo yako yanaendana na bajeti husika iliyotengwa kwenye hiyo nafasi.
Ikitokea mategemeo yako yanatofautiana kwa kiasi kikubwa basi mwajiri hana budi kuangalia watu wenye mategemeo yanayofanana au yanayokaribiana na bajeti iliyotengwa. Mfano. Kazi ya Afisa Tawala, mshahara wake ni 720,000 TZS kwa mwezi, halafu mategemeo yako ni 2,000,000 TZS, hapo itakuwa ni ngumu kufanya majadidliano na kufikia muafaka utakaokidhi matakwa ya kila upande.
Kwa wale wanaotafuta nafasi ya kazi ni vyema kuhakikisha kuwa unakuwa mkweli na muwazi. Usije ukadanganya tu ili upate kazi bali unatakiwa upate kazi itakayo kusaidia kutimiza malengo yako ya kikazi, kifedha na kimaisha kiujumla.
Vifuatavyo ni vitu muhimu vya kuzingatia wakati unapojibu swali la “Matarajio yako ya mshahra ni yapi?” (What are your salary expectations?):
Elewa vizuri kazi unayoenda kuifanya: Nasisitiza katika kusoma vizuri tangazo la kazi, uelewe majukumu ya kazi unayoenda kuifanya na matokeo unayotakiwa kusababisha. Ukishayatambua hayo utajua ni kiwango gani cha juhudi na kujituma kinachotegemewa kutoka kwako. Hapo utatakiwa ukadirie thamani ya muda, ujuzi na utaalamu wako na kiasi unachotakiwa kulipwa.
Fuatilia viwango mbalimbali vya mishahara kulingana na soko la kazi husika na eneo (market salary ranges): Kila kazi ina viwango vyake vya mishahara kulingana ujuzi, uzoefu na eneo/ nchi. Kazi ya Software Developer ukiwa Marekani kiwango chake cha mshahara ni tofauti na ukiwa Tanzania kutokana na kuwa tunatofautiana kiuchumi. Vilevile, kuna juzi ambazo mishahara yake ipo juu kulingana na kuwa uhitaji wake ni mkubwa kuliko zingine.
Jaribu kuzungumza na watu ambao walishawahi au ambao wanafanya kazi kwenye taasisi unayoenda kufanya usaili: Kama unaweza kuwafikia watu mbalimbali ambao wameshawahi kufanya kazi hiyo sehemu, nenda kazungumze nao. Hii siyo lazima.
Epuka kutaja kiwango cha juu au chini sana kupita kiwango: Kama utahitaji kulipwa mshahara mkubwa kupita thamani utakayoongeza uwe na uhakika waajiri watakuacha na huo ni utapeli. Vilevile epuka kutaja kiwango cha chini kwa sababu hautaweza kufikia malengo yako ya kifedha ambapo itakulazimu kutafuta kazi nyingine kama part-time job, freelancing n.k, kitu sera za kiutumishi kwenye maeneo ya kazi wanakataza au utalazimika kutafuta kazi nyingine ambayo inaathiri “career” yako kwa kile wanachooita ‘Kiguu na njia’ ama ‘Job Hopping’, yaani wewe kila siku upo barabarani na bahasha. Zingatia malengo yako ya kifedha, ujuzi wako na matokeo unayotakiwa kuyasababisha katika hiyo nafasi.
Zingatia manufaa mengine kama fursa za kujiendeleza, bima za afya, bonasi n.k: Muda mwingine tunatafuta kazi si tu kwamba tupate mishara bali tunataka kazi zetu ziwe sehemu ya kukua na kujiendeleza kwa kutupa uzoefu. Manufaa mengine yasiyo sehemu ya mshahara yanasaidia kufanya maamuzi kama kupewa bima ili kupata huduma za afya, bonasi kulingana na utendaji wa kazi, kamisheni, nafasi za kufanyia kazi ukiwa nyumbani (remote work).
Kuwa ‘specific’ na kiwango utakachotaja: Taja kiwango husika au kwa ‘range’ mfano. 750,000 TZS, au 670,000 – 800,000 TZS. Vilevile, taja kuwa ni mshahara kabla ya makato au baada ya makato (gross salary au net salary).
Onesha kuwa upo tayari kubadilika kuendana na viwango vya mshahara vya kampuni: Hii itakusaidia kuzingatiwa kulingana na uwezo wako ulioonesha na inakufanya kiwango cha mshahara ulichosema kisiwe kigezo cha kukutema.
Mifano mbalimbali juu ya namna ya kujibu hili swali (Kwa Kiingereza):
Mfano 1:
“My baseline salary requirement is $94,500. I feel that the value and expertise I can bring to this role support my compensation expectations. Is this in line with your thoughts?”
Mfano 2:
I’m expecting my salary to fall between …
“Let me start by reiterating how grateful I am for the benefits this job offers such as generous paid time off and health benefits. That being said, I am expecting my salary for this position to fall between $45,000 and $50,000 annually. My rich background in client services specific to this industry can play a role in strengthening the organization.”
Hayo ni baadhi ya mambo yanayoweza kukusaidia kufanya maamuzi wakati unapojibu swali la tuambie unataka kulipwa msharara kiasi gani (What are your salary expectations?). Zaidi ya yote kuwa mdadisi na jua thamani yako.
Niambie kama una changamoto za kushindwa usaili/ interviews, kuandaa wasifu wenye mvuto nami nitakusaidia!
Usiste kutufikia WhatsApp +255677904593 au email bettercareerproject@gmail.com